Sunday, October 14, 2018

Straika Kapera hana presha na Kagere, Eliud Ambokile



STRAIKA wa Kagera Sugar, Ramadhan Kapera ameangalia kasi ya ufungaji kwenye Ligi Kuu Bara na kutamka kwamba mambo yakiendelea kumnyookea atabeba tuzo ya ligi Mfungaji Bora wa ligi hiyo. Kapera huu ni msimu wake wa pili ambapo msimu uliopita aliichezea Majimaji iliyoshuka daraja amefunga mabao matatu na kuisaidia timu yake kushika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 12 baada ya kucheza mechi nane. Kwa idadi hiyo ya magoli, Kapera anaingia katika orodha ya wachezaji waliofunga mabao mengi msimu huu akiongozwa straika wa Mbeya City, Eliud Ambokile mwenye mabao sita huku 10/14/2018 Straika Kapera hana presha na Kagere, Eliud Ambokile -  Meddie Kagere wa Simba akiwa na mabao manne. Akizungumza na Mwanaspoti, Kapera alisema kutokana na mwanzo mzuri huenda mwisho wa ligi mambo yakawa mazuri pia kwake. Alisema mbali na kujituma, ushirikiano wake na wachezaji ndani ya timu pamoja na kufuata maelekezo ya Benchi la Ufundi anaamini atafikia malengo yake. “Namshukuru Mungu kwa kuwa tayari nimefikisha idadi hii ya mabao licha ya kwamba ligi ni ngumu, na lolote linaweza kutokea kwa sababu mbali na kujituma bado nina ushirikiano na wenzangu,” alisema Kapera. Mshambuliaji huyo aliongeza kuwa kwa sasa anajipanga na mbinu mpya kwani mabeki wa timu pinzani wakiona wanasumbuliwa na mshambuliaji wanakamini hivyo anabuni mbinu mpya ya kupenya ngome za mabeki wa timu pinzani. Alisema msimu huu ikiwa ni mara ya kwanza kukipiga Kagera Sugar anahitaji kuacha historia ndani ya timu hiyo ikiwa ni kuisaidia kumaliza katika nafasi nzuri. “Naendelea kupambana lakini kuwasoma mabeki wa timu pinzani ili kufikia malengo yangu, nataka niache historia hapa Kagera Sugar kwa kuiweka nafasi nzuri lakini nifunge mabao mengi,” alisema.
Share:

Popular Posts

Recent Posts

Categories

Text Widget

Pages